Monday, September 10th, 2007
Miss Tanzania 2007
Picha Adhia (pichani) binti wa miaka 19 tu anayeishi Kariakoo jijini Dar-es-salaam ndiye MISS TANZANIA 2007. Ameibuka mshindi katika mashindano ya Miss Tanzania yaliyofanyikia usiku wa jana katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar-es-salaam. Aliyeibuka mshindi wa pili ni Lilian Abel kutokea Kinondoni na wa tatu ni Queen David kutokea Temeke. Mmojawapo wa majaji wa mwaka huu alikuwa ni mnigeria Agbani Darego, mrembo wa dunia wa mwaka 2001. Tulipomhoji mwezi mmoja uliopita mara tu aliposhinda taji la Miss Kinondoni, Richa Adhia alitueleza mengi ikiwemo ndoto yake ya kushinda taji la Miss Tanzania na nini anatarajia kulifanyia taifa la Tanzania endapo atashinda. Sio vibaya kama tutajikumbusha tena mahojiano hayo.
Mashindano ya Miss World mwaka huu yanatarajiwa kufanyikia huko Sanya nchini China ndani ya ukumbi maarufu wa Crown Beauty Theater tarehe mosi(1)Decemba. Washiriki wanatarajiwa kuwa wameshawasili nchini China ifikapo tarehe 2 Novemba.
Picha zaidi na matokeo…
TOP THREE: Kutoka kushoto ni Queen David (Temeke), Richa Adhia (Kinondoni) na Lilian Abel (Kinondoni)
TOP TEN: Bila mpangilio maalumuLilian Abel, Gladness Katega, Richa Adhia, Cecilia Charles, Latifa Warioba, Queen David, Neema Khatibu, Victoria Martin na Hadija Sulla.
TOP FIVE: Kutoka kulia ni Richa Adhia, Victoria Martin, Lilian Abel, Hadija Sulla, Queen David.


